pspf

Jumatatu, 28 Desemba 2015

Diamond amwaga chozi Dar Live


Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo na kuwashangaza watu kufuatia mashabiki wake kumtaka awaimbie ‘akapela’ ya wimbo wake mpya wa Utanipenda.

Tukio hilo ambao bado limo midomoni mwa mashabiki wake, lilijiri usiku wa kuamkia Boxing Day (Desemba 26, 2015) ndani ya ‘Uwanja wa Taifa wa Burudani’ Dar Live jijini Dar ambapo nyota huyo alikuwa akikamua jukwaani na shoo ya nguvu iliyopewa jina la Funga Mwaka Concert.

Dakika chache kabla Diamond hajamwaga chozi, mashabiki wake walimuomba aimbe ‘akapela’ ya wimbo huo mpya.

Wakati akiimba akapela hiyo, mashabiki wake, bila kificho, walimwambia anajitabiria ‘kufulia’ kwani wimbo huo una kila alama za yeye kumaliza gemu la Bongo Fleva vibaya.

Hata hivyo, licha ya mashabiki kumpasulia hivyo, baadhi yao walianza kulia wakionekana kuguswa na mashairi ya wimbo huo hali iliyosababisha Diamond naye aanze kulia na kushindwa kuendelea kuuimba wimbo huo.

Kufuatia hali hiyo, dada yake kwa upande wa baba yake, Abdul Jumaa, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ alimfuata jukwaani na kumtoa huku akimfunika na kitambaa cha bendera ya taifa ambacho pia dada huyo alikitumia kumfutia machozi kaka yake huyo.

Diamond alipelekwa nyuma ya jukwaa ambako ukiachia mbali yeye Queen Darleen, meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ naye alitumia nguvu ya ziada kumbembeleza staa huyo huku akimwambia anawapa wasiwasi mashabiki wake. Kwa hiyo anyamaze.

Licha ya Babu Tale kutumia hekima ya kibabubabu, bado Diamond aliendelea kulia, safari hii kwa uchungu zaidi na kujiinamia huku akikataa kutulizwa wala kuambiwa maneno yoyote yanayoonekana ‘kama’ yana busara ndani yake.

“Huna sababu ya kuendelea kulia ndugu yangu kwani kufulia au kuendelea kuwa na mali ni neema na msimamo wa Mungu. Hakuna binadamu anayeweza kumshusha mwenzake kama Mungu hajapanga kuwa hivyo,” alisema Babu Tale lakini Diamond hakumsikiliza.

Diamond alinyamaza mwenyewe baadaye kufuatia mawasiliano ndani ya ubongo wake kumwambia ‘umelia sana kijana, imetosha sasa’!

Kilio hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku hiyo katika kumbukumbu.
 
Wimbo wenyewe uliomliza Chibu huu hapa


Vijana takribani 1500 mkoani Iringa wajitangaza kuwa Mashoga


Kukithiri  kwa biashara haramu ya ngono pamoja na tabia ya ushoga mkoani Iringa kunadaiwa kusababishwa na baadhi ya vijana wa vyuo vikuu waonafika mkoani humo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu, huku miongoni mwao wakitaka starehe zilizo nje ya uwezo wao.

Tamaa ya kumiliki vitu vya thamani – ni miongoni mwa mambo yanayotajwa  kuwahadaa baadhi ya wasomi hao wa vyuo vikuu, jambo linalosababisha wengi wao kuangukia katika wimbi la biashara ya ngono na ushoga na kuufanya  ongezeko la maambukzi ya vvu.

Kwa mkoa wa iringa inadaiwa kuwa zaidi ya mashoga 1500 wamejitangaza wenyewe kuendesha  biashara haramu ya ngono, jambo ambalo kiafya linadaiwa kuwa ni hatari  kwa maambukizi ya virus vya ukimwi.

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu  mkoani iringa ndiyo wanaonyooshewa kidole kuhusika na biashara hiyo ya ngono na tabia ya ushoga- ambapo shirika la restless development linalojihusisha na masuala ya afya ya uzazi na makuzi kwa vijana- kupitia mradi wa dance for life- limewakutanisha viongozi hawa wa serikali ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa- ili  kujadili namna ya kujinasua katika wimbi hilo la ushoga na biashara haramu ya ngono.

Serikali inaona  tatizo hilo la ushoga na biashara ya ngono litamalizwa na jamii yenyewe, endapo tu wazazi na  walezi watakemea mapema mienendo hatarishi ya vijana wao.

Ushoga ni tabia inayofanywa na baadhi ya wanaume, kwa  kujihusisha kimapenzi na wanaume wenzao, suala  ambalo kwa kiwango kikubwa linatajwa kuchochewa na mambo ya utandawazi, ambao unaibua mitindo mbalimbali na tabia mpya kila uchwao.

Chanzo :Star tv