pspf

Jumatatu, 28 Desemba 2015

Diamond amwaga chozi Dar Live


Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo na kuwashangaza watu kufuatia mashabiki wake kumtaka awaimbie ‘akapela’ ya wimbo wake mpya wa Utanipenda.

Tukio hilo ambao bado limo midomoni mwa mashabiki wake, lilijiri usiku wa kuamkia Boxing Day (Desemba 26, 2015) ndani ya ‘Uwanja wa Taifa wa Burudani’ Dar Live jijini Dar ambapo nyota huyo alikuwa akikamua jukwaani na shoo ya nguvu iliyopewa jina la Funga Mwaka Concert.

Dakika chache kabla Diamond hajamwaga chozi, mashabiki wake walimuomba aimbe ‘akapela’ ya wimbo huo mpya.

Wakati akiimba akapela hiyo, mashabiki wake, bila kificho, walimwambia anajitabiria ‘kufulia’ kwani wimbo huo una kila alama za yeye kumaliza gemu la Bongo Fleva vibaya.

Hata hivyo, licha ya mashabiki kumpasulia hivyo, baadhi yao walianza kulia wakionekana kuguswa na mashairi ya wimbo huo hali iliyosababisha Diamond naye aanze kulia na kushindwa kuendelea kuuimba wimbo huo.

Kufuatia hali hiyo, dada yake kwa upande wa baba yake, Abdul Jumaa, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ alimfuata jukwaani na kumtoa huku akimfunika na kitambaa cha bendera ya taifa ambacho pia dada huyo alikitumia kumfutia machozi kaka yake huyo.

Diamond alipelekwa nyuma ya jukwaa ambako ukiachia mbali yeye Queen Darleen, meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ naye alitumia nguvu ya ziada kumbembeleza staa huyo huku akimwambia anawapa wasiwasi mashabiki wake. Kwa hiyo anyamaze.

Licha ya Babu Tale kutumia hekima ya kibabubabu, bado Diamond aliendelea kulia, safari hii kwa uchungu zaidi na kujiinamia huku akikataa kutulizwa wala kuambiwa maneno yoyote yanayoonekana ‘kama’ yana busara ndani yake.

“Huna sababu ya kuendelea kulia ndugu yangu kwani kufulia au kuendelea kuwa na mali ni neema na msimamo wa Mungu. Hakuna binadamu anayeweza kumshusha mwenzake kama Mungu hajapanga kuwa hivyo,” alisema Babu Tale lakini Diamond hakumsikiliza.

Diamond alinyamaza mwenyewe baadaye kufuatia mawasiliano ndani ya ubongo wake kumwambia ‘umelia sana kijana, imetosha sasa’!

Kilio hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku hiyo katika kumbukumbu.
 
Wimbo wenyewe uliomliza Chibu huu hapa


Vijana takribani 1500 mkoani Iringa wajitangaza kuwa Mashoga


Kukithiri  kwa biashara haramu ya ngono pamoja na tabia ya ushoga mkoani Iringa kunadaiwa kusababishwa na baadhi ya vijana wa vyuo vikuu waonafika mkoani humo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu, huku miongoni mwao wakitaka starehe zilizo nje ya uwezo wao.

Tamaa ya kumiliki vitu vya thamani – ni miongoni mwa mambo yanayotajwa  kuwahadaa baadhi ya wasomi hao wa vyuo vikuu, jambo linalosababisha wengi wao kuangukia katika wimbi la biashara ya ngono na ushoga na kuufanya  ongezeko la maambukzi ya vvu.

Kwa mkoa wa iringa inadaiwa kuwa zaidi ya mashoga 1500 wamejitangaza wenyewe kuendesha  biashara haramu ya ngono, jambo ambalo kiafya linadaiwa kuwa ni hatari  kwa maambukizi ya virus vya ukimwi.

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu  mkoani iringa ndiyo wanaonyooshewa kidole kuhusika na biashara hiyo ya ngono na tabia ya ushoga- ambapo shirika la restless development linalojihusisha na masuala ya afya ya uzazi na makuzi kwa vijana- kupitia mradi wa dance for life- limewakutanisha viongozi hawa wa serikali ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa- ili  kujadili namna ya kujinasua katika wimbi hilo la ushoga na biashara haramu ya ngono.

Serikali inaona  tatizo hilo la ushoga na biashara ya ngono litamalizwa na jamii yenyewe, endapo tu wazazi na  walezi watakemea mapema mienendo hatarishi ya vijana wao.

Ushoga ni tabia inayofanywa na baadhi ya wanaume, kwa  kujihusisha kimapenzi na wanaume wenzao, suala  ambalo kwa kiwango kikubwa linatajwa kuchochewa na mambo ya utandawazi, ambao unaibua mitindo mbalimbali na tabia mpya kila uchwao.

Chanzo :Star tv




Jumatano, 16 Septemba 2015

Uapisho wa Mabalozi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Bi. Victoria Richard Mwakasege aliyekuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi. Balozi Victoria R. Mwakasege anaiwakilisha Tanzania nchini Malawi. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 16 September, 2015
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa  Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Zuhura Bundala kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais (Diplomasia) anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Samweli Shelukindo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Innocent E. Shiyo kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara hiyo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Afisa Ubalozi Mkuu, Ubalozi wa Tanzania, Muscat, Oman, Bw. Abdallah Kilima kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ubalozi wa Tanzania, Kampala, Uganda Bi. Anisa Mbega kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Mratibu wa Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Bw. Baraka H. Luvanda kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 

PSPF: FAHARI YA TANZANIA

Public Service Pension Fund ni moja ya mifuko kwa ajili ya pensheni kwa wafanyakazi serekalini.

Mfuko huu ni moja ya mifuko mbalimbali hapa Tanzania ambayo imejitahidi sana kujenga uchumi wa nchi hii.
 Hivi karibuni tumeshuhudia vichonga anga pacha, viwili katika maeneo ya Sokoine, jijini Dar es Salaam.
Ni majengo pacha yanayomilikiwa na mfuko huu, almaarufu kama 'PSPF Towers '....
Kusema kweli imeweza kupendezesha jiji la Dar na ni moja kati ya majengo marefu zaidi Afrika, vilevile jengo refu zaidi Afrika mashariki na kati.

Majengo hayo yanasemwa kuwa na urefu wa mita 147!!
Hebu pata kuona picha mbalimbali za jengo hilo lenye kuvutia...


Hii ni mpango wa jengo hilo kabla ya kujengwa...



Katika harakati za Ujenzi....


 Muonekano mpya wa jiji la Dar es Salaam....

 Naam... ni jioni njema kabisa majengo haya yakiangaza kwa mwanga maridadi..... Tanzania 

Kama mapacha........ watadumu daima..... Anga la Tanzania wanalipendezesha....
#VivaTanzaniaViva


Naomba kuwasilisha....
Eric Mangesho Jimmy.





LISSU AMJIBU JK KUHUSU RICHMOND



Morogoro/Dar. Siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amtaje mhusika wa Richmond anayezunguka naye kwenye kampeni, Mbunge huyo wa Singida Mashariki ameibuka na kudai kuwa Rais huyo ndiye mhusika kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kuteua na kuwawajibisha mawaziri.
Juzi, akiwa Kigoma, Rais Kikwete alieleza kumshangaa Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati
 mtu huyo anazunguka naye kwenye mikutano ya kampeni na kumtaka amtaje la sivyo yeye (Rais), atamtaja.
Akihutubia mkutano wa kumnadi mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, mwanasheria hiyo alianza kwa kusema: “Sasa ndugu zangu naomba leo nimjibu Kikwete na tumalizane na hii habari ya Richmond.

Alisema mkuu huyo wa nchi 
ndiye mhusika kutokana na 
mamlaka yake na; “si ya huyu Lowassa anayedai natembea naye kwenye kampeni. Hapa kwenye mkono wangu nina taarifa ya mwaka 2008 ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Richmond, Dk Harrison Mwakyembe, sasa ni miaka 
zaidi ya saba tangu isomwe 
bungeni.”
Lissu aliyekuwa akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege, alinukuu maelezo ya taarifa ya Mwakyembe kifungu kwa kifungu na kueleza namna ambavyo taarifa hiyo haikuweza kumtia hatiani Lowasa, bali aliwajibika kutokana na makosa ya watendaji wake.


Baada ya kueleza kwa kina taarifa hiyo, Mwanasheria huyo alisema Rais Kikwete ndiye pekee mwenye mamlaka ya kuwateua mawaziri, akisema alimteua Nazir Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha na ndiye mwenye mamlaka ya kuwawajibisha. Karamagi na Dk Msabaha walikuwa wameshika uwaziri wa Nishati na Madini kwa nyakati tofauti wakati wa sakata la Richmond na walijiuzulu pamoja Lowassa.


“Waziri mkuu Lowassa baada ya
 kutokea kwa sakata hilo alimwendea Rais Kikwete na kumweleza kuwa ‘kimenuka’ tuvunje mkataba baada ya wabunge wa upinzani kuchachamaa kuhusu sakata hilo, lakini alikataa na kumweleza kuwa hizo kelele za wapinzani zitaisha tu,” alisema.
Alisema baada ya Lowassa kujiuzulu mwaka 2008, tayari mashine za kutengeneza umeme zilishafika nchini na baada ya kujiuzulu haikufahamika zilikokwenda na kwamba baadaye mkataba wa Richmond ukahamishiwa kwa kampuni ya Dowans ambayo iliendelea kulipwa mabilioni ya shilingi.

Alimtaka Rais Kikwete awaambie Watanzania kwa nini Serikali yake iliendelea kuilipa Dowans mabilioni ambayo ilikuwa ya mfukoni na kwamba kama Lowassa alifanya makosa kwa nini hajapelekwa mahakamani kwa miaka minane tangu ajiuzulu.
“Rais Kikwete asitake kumaliza hizi siku chache za kampeni zilizobaki kwa shari na mimi na naomba niwaambie, Lowassa amefanya kazi katika umri wake wote wa miaka 62 ndani ya CCM na Serikali yake, lakini ameamua kuhamia huku kwa ajili ya kuleta mabadiliko na kuacha marupurupu yake yote,” alisema Lissu.


Lowassa apotezea

Aliposimama kuhutubia mkutano huo, Lowassa hakugusia kabisa suala hilo la Richmond na badala yake akaahidi iwapo atachaguliwa, serikali yake itafanya kila linalowezekana kuanzisha benki maalumu ya maendeleo kwaa ajili ya mama na baba lishe, vijana wa bodaboda na wamachinga ambao alisema watakuwa ni marafiki wakubwa wa serikali yake.

Alieleza kufurahishwa na umati huo akisema umemkumbusha siku alipowasili mkoani hapa kutafuta wadhamini, kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM.

Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye aliwataka wananchi kutobabaishwa na vitisho vinavyotolewa na viongozi wa CCM kuwa upinzani ukiingia Ikulu kutakuwa na machafuko.


Alisema serikali ya Ukawa ikiingia madarakani itahakikisha inasimamia mambo iliyoyaainisha kwenye ilani ya uchaguzi, tofauti na serikali ya CCM ambayo mbali na kuahidi maisha bora na kukusanya kodi za wananchi, bado hali imeendelea kuwa mbaya siku hadi siku.

Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema Morogoro Mjini, Albanie Marcos aliahidi kusimamia viwanda mjini hapa vikiwamo vilivyobadilishwa matumizi, kurudi kuwa chini ya wananchi.

Kauli za wadau
Wakizungumzia kauli ya Rais Kikwete kuhusu Richmond, baadhi ya wasomi na wadau wa siasa nchini walisema hayo ni malumbano ya kisiasa.
Profesa Michael Ndashau wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kauli za kulumbana kuhusu sakata la Richmond ni kufurahisha genge, kwa sababu kila siku maneno ni hayohayo.Alimtaka Lissu kuweka bayana uthibitisho wa uhusika wa Rais mbele ya jamii ili wananchi wapate la kuamini.
“Lissu kasema, Kikwete kajibu, malumbano yanabaki palepale, mwenye nafasi nzuri ya kusema tena ambaye yupo upinzani ni Lissu, aeleze kwa ushahidi ili ambane mhusika maana bila uthibitisho yatakuwa yaleyale kulumbana bila kufikia mwisho.


Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema wote wawili wanaufahamu ukweli. Alisema hizo ni hadaa lakini hakuna kati yao asiyemfahamu mtuhumiwa wa Richmond, “Rais ametoa uhuru kwa Lissu amtaje, hivyo kama anamfahamu afanye hivyo, lakini anafahamika na siyo Baregu, Slaa wala Mbowe, wote wanamfahamu,” alisema Dk Bana.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo Bisimba alisema hilo siyo suala la Rais kumuagiza Lissu, bali alitakiwa afanye mwenyewe kwa sababu anayo haki ya kufanya hivyo.


“Rais kupitia vyombo husika ndiyo anatakiwa atoe amri mhusika achukuliwe hatua kama anamfahamu, ana kila sababu ya kufanya hivyo, kama alikaa kimya wakati huo, wakati huu haitasaidia?” alisema Bisimba.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi alisema kujadili suala hilo sasa ni kuwanyima wananchi uhuru wa kujadili mambo ya msingi yenye tija kwa Taifa.


Jumanne, 15 Septemba 2015

Jaguar...... F PACE yavunja rekodi mpya ya kuzunguka mduara wa nyuzi 360

                  Gari la kampuni ya Jaguar limefanikiwa kuingia katika vitabu vya  historia baada ya kuweka historia ya kipekee kwa mara ya kwanza baada ya kuzunguka mzunguko 'loop the loop' wenye meta 19.08... mduara huo ulikuwa ni wa nyuzi 360. Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva maalum, na dereva huyo alifanikiwa kudhibiti gari hilo kutokuathiriwa na nguvu ya mvutano. Guinness World records Imethibitisha.

Bofya hapo chini kuona video ya tukio hilo